Featured
Loading...

THE MOMENTS WHEN WE LOST OUR BELOVED

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


Rafiki wa mpendwa wetu Catherine Nyongole akishindwa kujizuia mara tu alipomuaona mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera(kilemba chekundu) alipofika nyumbani kwa marehemu kutoa pole na kujumuika nao katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao Zainab Buzohera aliyefariki jana jioni Jan 4, 2014 katika hospitali ya Doctor's Community iliyopo Goodluck Rd, Lanham, Maryland. Msiba upo nyumbani kwa wafiwa 5030 57th Ave, Bladensburg, Maryland na leo baadae kutafanyika harambee ya kuchangisha fedha ilikusaidia kuusafirisha mwili wa marehemu harambee itafanyika 5401 Anapolis Rd, Bladensburg, Marland kuanzia saa 10 jioni(4pm) Lengo ni kujitahidi kumsafirisha mpendwa wetu siku ya Jumatano Jan 8, 2014.Watanzania wakiamua hawashindwi na jambo.
Watanzania wa DMV wakijumuika na wafiwa nyumbani kwa marehemu.
Catherine Nyangole mwenye kilemba cheusi pamoja na WanDMV wakimpa pole mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera nyumbani kwa marehemu.
Watanzania wa DMV wakiendelea kutayarisha makulaji kwa ajili ya wageni watakaofika nyumbani kuwapa pole wafiwa.
Watanzania DMV wakijumuika pamoja na wafiwa nyumbani kwao
Watanzania wa DMV wakiwafariji wafiwa.
Mfiwa kushoto Bw.Dula ambaye ni mume wa marehemu akiwa na Terry katika msiba huo Jumamosi usiku huko Bladensburg Maryland pamoja na Tery Watanzania wa DMV waliungana pamoja na familia usiku huohuo wa jana mara baada ya kupata taarifa ya msiba. Msiba upo nyumbani kwa marehemu 5030 57 th ave Apt 303 Bladensburg md 20710Mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera (wa pili kulia)akiwa amezungukwa na jamaa, ndugu na marafiki wakimfariji.walipojumuika jioni mara baada ya kupata taarifa ya msiba wa mpendwa wao Zainab Buzohera aliyefariki jana jioni Doctor's Community Hospital iliyopo Lanham, Maryland,
Mume wa marehemu Dullah (tshirt nyekundu) akifajijiwa na Watanzania DMV waliofika nyumbani kwao 5030 57 th ave Apt 303 Bladensburg md 20710 usiku huo mara tu baada ya kupata taarifa ya msiba.
Ndugu, jamaa na marafiki wakisoma dua nyumbani kwa marehemu Bladensburg, Maryland
Watanzania DMV wakijumuika pamoja nyumbani kwa marehemu kuwafariji ndugu,na jamaa wa marehemu mara tu walipopata taarifa ya msiba wa kufiwa na mpendwa wao.
Watanzania wa DMV wakijumuika pamoja na wafiwa nyumbani kwa marehemu.
Edward Taji akijumuika na wafiwa nyumbani kwao Bladensburg Maryland.
Alfan Limmo (kulia) pamoja Jabir Jongo wakiwa kwenye msiba wa mpendwa wetu Zainab Buzohera.

Images via Vijimambo

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top