Featured
Loading...

DIAMOND: My #1 REMIX ILIVYOMTENDA NA KILA KITU KUHUSU YEYE

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


Kipindi tunasikia habari kuwa Diamond amemlipa Davido kumshirikisha kwenye remix ya wimbo wake, My Number One, wengi walipata hofu kidogo na kuhisi haukuwa uamuzi sahihi. Walihisi huo haukuwa uamuzi sahihi kwakuwa tayari alikuwa ameshawekeza fedha nyingi kwenye video ya wimbo huo iliyofanyika nchini Afrika Kusini.


Mimi pia nilidhani ingekuwa vyema kama nguvu zote hizo angeziwekeza katika kufanya wimbo mpya kabisa na kuachana na remix ya My Number One ambayo tayari ilikuwa imeshafanikiwa. Baadaye nilisikia kuwa ni Davido ndiye aliyeupenda wimbo huo kati ya zile alizosikilizishwa na hivyo hakukuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivyo. Remix hiyo ilifanyika Tanzania na nahisi walienda kuimalizia Nigeria kwenye studio ya nyumbani ya Davido.


Akiwa Nigeria, Diamond alimtafuta muongozaji wa video anayekiki zaidi barani Africa, Clarence Peter kufanya video hiyo ambayo anasema ilimgharimu takriban dola 30,000. Video hii ina historia ya kuvutia na kama si washauri wake, alikuwa amepanga kutoitoa kabisa. Ndani ya muda mfupi, video hiyo ilikamilika na Clarence kumtumia Diamond mzigo ambao hata hivyo haukumridhisha na kumtaka muongozaji huyo kurekebisha baadhi ya vitu.
Wakati sasa yupo kwenye marekebisho huwezi kuamini bahati mbaya material yakafutika ikanichanganya ikawa tena hawezi akaapoligise ‘unajua imetokea bahati mbaya kwahiyo video haiwezi kubadilishwa tena inabidi iwekwe vile,
Diamond alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, mwanzoni mwa January.
“Nikakaa nayo ndani nikasema ‘hii video nifanyeje’ nisiitoe, niiache ama nifanya nini?. Lakini wenyewe akina Davido, akina nani wananimbia ‘ebana hii video kali sana Diamond let’s release it na nini’ kwasababu material yamefutika, I had no choice, nikakaa nayo kama wiki tatu hivi nikasema nafanyaje sasa’. Nikakaa na management ikasema ‘tuiachie tu video lakini watu wajue kuna tatizo hili na hili, so kutakuwa na mapungufu kidogo kwenye video ambayo hayakuwa ndani ya uwezo wetu,” aliongeza Diamond.
Mungu si Athumani, video ya msanii huyo imemletea neema pomoni na kumuongezea wigo zaidi na hivyo ‘kuwaprove wrong wale waliohisi hakufanya uamuzi sahihi. Kwa sasa remix ya My Number One ni miongoni mwa nyimbo kubwa zaidi barani Afrika iliyoshika chart za redio maarufu nchini Kenya, Uganda, Nigeria na kwingine.
“Sasa hivi My Number One imeingia kwenye chart za Afrika nzima, sio Tanzania peke yake,” Diamond ameiambia Bongo5.
Ukiangalia Trace ipo namba tano, ukiangalia Sound City ipo namba moja, ukiangalia mpaka BBC ipo namba tano na sehemu zingine chart tofauti tofauti. Zamani muziki wangu ulikuwa unafanya vizuri sana Afrika Mashariki lakini kwingine ulikuwa unafanya kwa kusuasua. My Number One imenipa issue nyingi tu kama kwenda kwenye awards Marekani (AFRIMMA Awards). Kwa mfano juzi kati tu hapa nilikuwa South Africa nafanya ngoma ya kilimo ambayo wameteuliwa wasanii wote wanaofanya vizuri kila nchi ambayo kwa Tanzania tulienda mimi na AY. Lakini mimi najua kabisa kuchaguliwa kwangu kumetokana na ile ngoma kwasababu wameiona kuwa kuna msanii wa Tanzania yuko hivi na hivi na kufuatilia details wakaona dah ‘kumbe mtu mwenyewe sio mtu mzuri’. That’s was my target, naona sasa inafanya vizuri sana kuliko hata nilivyofikiria mimi, nilijua haitafika hivyo. Nilijua itanipa airtime tu. Sasa hivi ukienda kama Ghana na sehemu nyingine, ni ngoma ambayo inapigwa na kuhit kama inavyohit sehemu zingine kama nyumbani, tofautisha na wasanii wetu wengi ambao ngoma zao hazihit yaani zinapigwa tu, lakini ngoma ile imehit.
Diamond anasema kwa sasa hata akizungumza na wasanii wakubwa wa Afrika, wanamchukulia kama msanii mkubwa mwenzao na heshima imeongezeka. “Kwanza wote ninaokutana nao wananijua kabla, tofauti na kuwaambia mimi ni fulani,” anasema.
Hadi waongozaji wa video, wao ndo wananifuata mimi na kusalimiana na mimi. Akina D’Banj, akina Wande Coal na watu wengi ambao wao kwanza wanafahamu kazi yangu mimi na kuappreaciate kazi yangu na kuisalute sana sio kwa kuniona ‘huyu naye nani kaja’ ni watu ambao wana heshima. Ndio maana hata katika project niliokuwa nao mimi nilikuwa napewa kipaumbele sana sababu ya kazi zangu ambazo zimesababisha niwe hivi. So wakitazama kazi halafu wakiangalia profile yangu, wakiangalia matukio yangu, wanaona ‘huyu mtu mkubwa’.
Amesema anayo miradi mingine mikubwa ya kimataifa itakayokuja hivi karibuni. “Nina project na Iyanya, nina project na D’Banj na wasanii wengine tofauti tofauti,” amesema. Ameongeza kuwa mwaka huu atatoa nyimbo mbili ambapo moja itakuwa kwaajili ya Afrika Mashariki na nyingine kwaajili ya Afrika Magharibi.
Nimeamua kufanya hivyo kwasababu, Watanzania tuna kawaida moja, ukiimba katika lugha ya kigeni au muziki wa aina ya kigeni ni ngumu sana Watanzania au East Africa kukupokea kwasababu wanaona kama ‘huyu vipi’. Na kule pia huwezi kuwaimbia muziki wa Kitanzania ukawapelekea so hauwezi kuhit kwasababu watakuwa hawakuelewi. Kwahiyo ntatoa ngoma mbili, ambayo moja target yake itakuwa ni East Afrika na nchi zingine duniani halafu ntakuwa na ngoma moja ya West Africa ili wasione kama ‘sasa mbona kabadilika ghafla’.
BY BONGO 5

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top