Featured
Loading...

MISS TABORA 2012 ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO NA KUFURAHIA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


Mrembo Sarah Paul aliposhiriki furaha yake ya siku ya kuzaliwa na watoto wa kituo cha TZ 820 FPTC NG'AMBO STUDENT CENTER - Kilichopo Tabora.
Mrembo huyo akiongea na watoto
Richard, mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha SAUT (SAUT-TABORA) AMUCTA anayesomea Mahusiano ya Umma na Masoko akiongea na watoto.
Miss Pauline (Mshindi namba 3 wa chuo cha Utumishi wa Umma-Tabora) akiongea na watoto.
Sarah akikata keki na watoto.
Kila mmoja alipata nafasi ya kufurahia keki iliyoandaliwa maalumu kwa watoto hao.
Baadhi ya vitu alivyowaandalia watoto hao na kuvikabidhi kwenye shirika hilo.
Suleiman H. Halletu (Mkurugenzi wa kituo) akishukuru baada ya kupokea zawadi za mrembo Sarah kwaajili ya watoto.
Team nzima iliyomsindikiza mrembo katika hafla hiyo fupi. Kutoka kulia ni Marry, Richard, Miss Zennah (Miss Singida 2012/13), Miss Pauline, Miss Sarah (MissTabora2012), Miss Lilian (Mshindi No2 TPSC 2013), na Annah Henry (Afisa Ugani)
Sarah Paul, mshindi wa shindano la urembo la Redds Miss Tabora 2012, ambaye pia mwaka jana alishiriki katika shindano hilo hadi kufikia fainali za Miss Tanzania.
****
Leo katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa amefanikiwa kuwatembelea watoto wanakusanywa na kanisa la FPCT NG'AMBO wanaopewa msaada na Shirika la Compassion International Tanzania na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto hawa wanakusanywa kwa lengo la kuwatoa na kuwakomboa umaskini wa kiuchumi, kijamii, kimwili na kiroho na kuwawezesha waje wawe watu wazima wanaojua wajibu wao na kujitegemea.
Pia huwalipia ada, huwauguza na kuwapeleka hosipitali wanapoumwa, huwafundisha ujasiriamali n.k Aliyasema  Suleiman H. Halletu mkurugenzi wa kituo kinachoitwa TZ 820 FPCT NG'AMBO STUDENT CENTER na kuongeza kuwa wana watoto 254 katika kituo chao.

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top