Featured
Loading...

BAADA YA DOGO JANJA KUTAKA KURUDI TIP TOP BABA YAKE MZAZI AFUNGUKA JUU YA SWALA HILO

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE



Alhamisi ya March 20 2014 lilitoka tamko ambalo lina maamuzi ya msanii wa bongofleva Dogo Janja kuhusu kuomba msamaha na kuhitaji kurudi kwenye kundi lake za zamani la Tiptop connection na kuyasahau yaliyopita kati yake na aliyekuwa meneja wake pia ambae ni Madee. Stori hii ina pande nyingi sana ambazo zitazungumza kupitia hapahapa kwenye tovuti hii lakini kwa kuanzia, baba mzazi wa Dogo Janja amepata nafasi kuzungumza kwa mara ya kwanza baada ya mtoto wake kuomba msamaha.
Anasema
Dogo Janja alishakua mtu mzima na tayari nilishawahi kumwambia achague mahali atakapoona kuna manufaa kwake, akishafanya maamuzi yake huwa ananishirikisha kwenye kujadiliana, tayari alishawahi kuniambia kuwa atafanya maamuzi baada ya kuona Mtanashati hakuna muelekeo wowote na hakuna anachopata ndipo akaniambia baba mimi mtu yoyote au kundi lolote nitakalokubaliana nalo basi nitafanya nao kazi.
Hayo ni maelezo ya Baba mzazi wa Dogo Janja ambae ametoa baraka zote kwa Janja kurudi kujiunga na Tiptop Connection hivyo kazi imebaki kusikia kutoka upande wa Tiptop kufahamu kama wameukubali msamaha wa Dogo Janja.

Source: Milard Ayo

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top