
Mr Blue. Msanii ambaye amejitia aibu mwenyewe kwa wanyamwezi na Watanzania kwa ujumla kwa kile kilicho daiwa kutaka kufanya urubuni wa pesa akihisi unyamwezi (Ujanja) ni Dar na mikoa mingine, la hasha mambo yote kinyume na fikra zake.

Pamba alizozinyuka Mr Blue ambazo zilikuwa hazijalipwa.

.......
Baada ya fununu kusambaa na kuwa ni story ya mji pande za Wanyamwezi mkoani Tabora karibu kila kona mtandao wa aloyson.com uliamua kufuatilia suala hili kwa undani kwa kumvutia uzi [simu] mhusika aliyewekwa kwenye target ya kuibiwa pamba hizo zenye gharama ya kama 150,000.
Ni kweli alitaka kusepa na mkwanja kama wa 150,000/= ambazo kila ulichoona kavaa mie ndiye nilimkopesha kwani alidai hajapewa pesa yake ya show na kwa kuwa kaahidi kuwa siku baada ya show atakuwepo na ataileta pesa hiyo basi nikamuachia,
Cha ajabu nilipigiwa simu na msamaria mwema mida ya alfajiri baada ya show na kupewa taarifa kuwa jamaa anajiandaa kusepa, sikuchelewa nikafika hotelini alipofikia nikamkuta akijiandaa na kwa mtiti pesa ikalipwa..... Alisema Chura Fashion mmiliki wa duka hilo la pamba