
Dawati letu za habari leo asubuhi mapema limepokea taarifa za kusikitisha toka maeneo ya Kipunguni - Ukonga jijini Dar salaam ikihusiana na ajali ya moto (pichani) iliyoua watu sita wa familia moja ya Mzee Mpila.
Chanzo cha habari kimetaja marehemu hao ni baba na mama wa familia hiyo, ndugu wa baba wa familia hiyo, mtoto mmoja wa familia hiyo pamoja na wajukuu wawili wa familia hiyo.
Majirani wamesema walikisia kelele za za wajukuu wakiita Bibi moto na kelele za mtoto wa familia hiyo Lucas akiita baba moto hadi sauti hizo zilipopotea masikioni mwa watu. Inasemekana pia Mwanafamilia mmoja anafahamika kwa jina la Ima alifanikiwa kujiokoa katika ajali na kifo hicho.
Hadi sasa chanzo cha moto hakijafahamika ila Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam aliweza kutembelea eneo la tukio majira ya saa nane mchana wa leo.
Mazishi ya Marehemu hao yanatarajiwa kufanyika siku ya jumanne katika makaburi ya Airwing huko Banana - Ukonga