
WhatsApp ni mtandao ambao kwa hivi karibuni zilitolwa takwimu zinazothibitisha kuwa ni mtandao unaoongoza kwa watumiaji wengi kwa kusafirisha jumbe zao au meseji kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine pamoja na makundi.
Inafikia hatua wakati mwingine meseji za makundi hukera na kwa bahati mbaya wawezajikuta umeunganishwa tu kwenye makundi ambapo yanaweza kukuondolea umakini katika shughuli zako kwa wingi wa meseji watumianazo wanakundi husika. Si kila kundi halina faida, yapo makundi yenye mikakati mizuri na wanafanikisha malengo mengi kwa misingi yao ya kundi husika.

Hivyo kwasasa ukitaka kukwepa usumbufu wa kelele za meseji za kila wakati unaweza ku-MUTE taarifa za jumbe zote za WhatsApp, mfano katika makundi hadi kufikia miaka 100 kama inavyonesha katika picha. Simu zilizo nyingi utakuta inaonesha MUTE hadi ya mwaka mmoja bali kadri unavyozidi ku-UPDATE application hiyo itakuruhusu ku-mute kwa miaka mia moja.