Featured
Loading...

Mourinho na Kashfa Nzito ya Uropokaji; Arekodiwa Kisiri; Soma Zaidi Hapaaa........

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE





Jose Mourinho kocha wa Chelsea FC na mshambuliaji wa timu hiyo Samuel Eto'o chini

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amejikuta akikukamilisha msemo wa Nyani haoni kundule pale aliporekodiwa akiwaponda washambuliaji wake na chaneli ya Tv Canal plus ya Ufaransa. Mourinho aliyekuwa akisubiri kuhojiwa na chaneli hiyo alikuwa akiongea na mfanya biashara wa Ki
Swizi alirekodiwa akimwambia "Tatizo la Chelsea sina washambuliaji" kisha akaongeza "Nina Eto'o lakini ana miaka 32" Au pengine 35 nani ajuae? Canal plus bila kufanya ajizi wakarusha hewani kauli yake hiyo pale timu yake inapojiandaa na mchezo muhimu dhidi ya Galatasaray utakaochezwa kesho nchini Uturuki, jambo liliompelekea Mourinho kukasirika na kudai Canal plus hawana weledi wa kazi waliporekodi mazungumzo binafsi na kuyarusha hewani.

Kwa maoni yangu tu Mourinho hapaswi kuzungumzia weledi pale ambapo yeye mwenyewe ni bingwa wa choko choko hasa kwa makocha na wachezaji wa vilabu vingine, siku hiyo hiyo alirekodiwa pia akimzungumzia Radamel Falcao ambaye ni mshmbuliaji wa klabu Monaco alikaririwa akisema 
"Falcao anahitaji timu na Chelsea inahitaji Mshambuliaji, akaongeza mchezaji kama yeye hawezi kucheza mbele ya watazamaji 3000 tu" akimaanisha Monaco haina watazamaji wengi kitu ambacho bila shaka viongozi na washabiki wa Monaco watakerwa sana na kauli hiyo. Hivyo basi Jose Mourinho aache kulalama 
"He should get on with it" kama Waingereza wasemavyo![Imeandikwa na http://keronyingi.blogspot.com/]

habari na picha kwa hisani ya dailystar

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top