Ommy Dimpoz ambae amerudi nchini hivi karibuni kutoka London ambapo alikua ameenda kwa ajili show 2 na kushoot Video chini ya usimamizi wa Gonga Entertainment. Katika Picha Ommy Dimpozanaonekana ameshikiliwa na Metropolitan Police wa nchini uingereza na hii ni moja kati ya scene ambayo imetumika katika Video ya Nyimbo yake mpya iliyotengenezwa na Director Mr Moe Musaambaye amefanya kazi nyingi sana na kubwa za wasanii wa Uingereza na Nigeria kama Azonto yaFuse ODG.
Video hii inatarajiwa kumalizika na kuachiwa mwishoni mwa mwezi huu ambayo inatarajiwa kuwepo kwenye chanel nyingi na kubwa kutokana na Director na ufanyaji wa Video hii ambapo vifaa vilivyotumika ni modern na vyenye gharama ya juu sana ikiwemo Camera RED pamoja na professional FILM crew waliotumika kushoot video hii.
Video hii imemgharimu OMMY Dimpoz si chini $20,000 za kimarekani ambazo ni kiasi pekee alichomlipa Director huyo na hiyo ukitoa gharama zake nyingine zilizotumika kwenye kusafiri pamoja na kuwepo nchini Uingereza kwa kipindi kizima cha utengenezaji wa video hiyo.