
Hicho kijumba ni moja ya vijumba kadhaa vya moja ya vyuo vya kilimo vya serikali hapa nchini Tanzania. Hiki ni chuo kinachotoa mafunzo ya kilimo kwa ngazi ya cheti na stashahada, na nchi yetu tunaamini na ipo hivyo kuwa uti wetu wa mgongo ni kilimo. Hali si shwari ikiwa wasomi wetu wanapitia mazingira kama haya, tunajidanganya wenyewe kabisa kwani hivi sasa hata mnyama wa kufugwa hana hadhi ya kuishi humo. Haipingwi kuwa moja ya uzalendo ni kukubali kile ulichonacho na kikakutosheleza kujisifia kwa hicho ulichonacho ila si kwa mtindo huu.

Yaonekana hata wanavyuo wenyewe waishio humu ni watu wenye fikra zenye itikadi zao ukizingatia majina ya milango yao "GORILLA KILLER"


Unapata picha gani majina kama haya "NEW PALESTINA"
*SI MABWENI YOTE NI MABAYA YAPO MAZURI PIA LAKINI UKIANGALIA HUPATI UWIANO WA HALI HALISI NA VIJUMBA HIVYO"
Mtandao huu haujafanikiwa kufanya tafiti kwenye vyuo vingine na yawezekana hali si shwari kabisa na afadhali ya hapo
Kwa mdau mpenda mabadiliko anitumie picha kupitia email: aloyson@live.com