Featured
Loading...

MH RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JOHN POMBE MAGUFULI AHUUHUTUBIA MAMI YA WANANCHI WA TABORA JULAI 24,2017

Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt John Pombe Joseph Magufuli,akihutubia mamia yawananchi wa Mkoa wa Tabora Kwenye Uwanja wa Mpira
wa Alli Hassani MwinyiJulai 23,2917.

Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt John Pombe Joseph Magufuli,akihutubia mamia yawananchi wa Mkoa wa Tabora Kwenye Uwanja wa Mpira
wa Alli Hassani MwinyiJulai 23,2917.

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Pombe Yahusishwa, Ajali Mbaya ya Bodaboda..! Askari Nao Jee..?

Kamera ya mtandao huu imelimulika tukio baya la ajari iliyohusisha pikipiki mbili eneo la Club Royal karibu na lango la kuingilia chuo cha Utumishi wa Umma cha Tabora zamani UHAZILI.
Mfuatiliaji wa tukio alibainisha dereva mmoja alikuwa anatokwa na harufu ya pombe kitu kilichodhihirisha kuwa alikuwa amelewa huku kamchukua abiria na akiendesha chombo cha moto.
Mashuhuda waliuambia mtandao huu kuwa wanalalamikia jeshi la polisi kuto kujitokeza mapema eneo la tukio licha ya kuwa hapana umbali unaozidi mita 100 kutoka eneo la tukio, mfuatiliaji wa tukio aliwahoji kama kuna yeyote aliyetoa taarifa kituoni dhidi ya tukio hilo lakini hakupata majibu.
Kasendeka, mhanga wa ajali iliyohusisha pikipiki mbili maarufu kama bodaboda.  
Kasendeka, mhanga wa ajali iliyohusisha pikipiki mbili maarufu kama bodaboda eneo ilipo Club Royal karibu na lango kuu la kuingilia Chuo Cha Utumishi cha Tabora zamani kikifaahamika kama UHAZILI.
Kasendeka akiwa anazinduka ziduka, akili inakuja baada ya kuzimia kwa muda kidogo kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki mbili eneo la ilipokuwa Club Royal.  
Kasendeka akiwa anazinduka ziduka, akili inakuja baada ya kuzimia kwa muda kidogo kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki mbili eneo la Club Royal karibu na lango/ geti la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI.
Ajali-bodaboda-tabora (5) Abiria na mhanga wa ajali hiyo akiwa anaugulia maumivu baada ya ajali iliyotokea muda mfupi maeneo ya Club Royal karibu na geti kuu la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI  
Abiria na mhanga wa ajali hiyo akiwa anaugulia maumivu baada ya ajali iliyotokea muda mfupi maeneo ya Club Royal karibu na geti kuu la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI
Ajali-bodaboda-tabora (2) Ajali-bodaboda-tabora (3) Mashuhuda wa tukio la ajali iliyohusisha pikipiki mbili maeneo ya Club Royal  
Mashuhuda wa tukio la ajali iliyohusisha pikipiki mbili maeneo ya Club Royal
Kasendeka akiwa anaangalia pikipiki yake baada ya ajali hiyo muda mfupi alipozinduka.  
Kasendeka akiwa anaangalia pikipiki yake baada ya ajali hiyo muda mfupi alipozinduka.
Askari wa Jeshi la usalama barabarani akijongea eneo la tukio. Inakadiriwa ni zaidi ya dakika 15 au zaidi zilipita ndipo askari alijitokeza eneo la tukio licha ya tukio hilo kutokea umbali wa mita za makadirio zisizozidi 100.  
Askari wa Jeshi la usalama barabarani akijongea eneo la tukio. Inakadiriwa ni zaidi ya dakika 15 au zaidi (Kwa mujibu wa mashuhuda) zilipita ndipo askari alijitokeza eneo la tukio licha ya tukio hilo kutokea umbali wa mita za makadirio zisizozidi 100 kutoka kituo kukuu cha Polisi mjini Tabora.
Askari akifuatilia tukio hilo baada ya dakika zinazokadiriwa na mashuhuda wa tukio kuwa ni zaidi ya 15 toka ajari imetokea.  
Askari akifuatilia tukio hilo baada ya dakika zinazokadiriwa na mashuhuda wa tukio kuwa ni zaidi ya 15 toka ajari imetokea.
Askari akimhoji Kasendeka kabla ya kwenda naye kituoni huku mhanga mmojawapo kuwa tayari alishakimbia eneo la tukio na kuisaliti pikipiki eneo la tukio.  
Askari akimhoji Kasendeka kabla ya kwenda naye kituoni huku mhanga mmojawapo kuwa tayari alishakimbia eneo la tukio na kuisaliti pikipiki eneo la tukio.
Ajali-bodaboda-tabora (1)  
Picha na Aloyson
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Umeipata Hii....? Kweli Kufa Kufaana; Gari La Kipekee La Jeneza Lawasili Nchini..!

Kwa wanaohitaji kukodi kwa shughuli za misiba wanaweza kuwasiliana kupitia barua pepe kiwiaadavidson@hotmail.com au

simu namba +255 715 213213, +255 713 616606 na +255 784616606

gari-la-kubebea-majeneza
Pichani juu na chini ni muonekano wa Gari maalum la kukodisha kwa ajili ya shughuli za kubebea majeneza katika misiba limeingia nchini.
gari-la-kubebea-majeneza gari-la-kubebea-majeneza
Muonekano wa ndani sehemu maalum linapowekwa jeneza.
gari-la-kubebea-majeneza
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MSIMU MPYA WA KANDANDA NDANI YA DSTV KUTIMUA VUMBI WIKI IJAYO.

IMG_0388
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa msimu mpya wa kandanda kwa wateja wa DStv jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
IMG_0397
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma za DStv. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi.
IMG_0422
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu, akielezea huduma za kuunganishwa kwa wateja wapya wa DStv, ambapo ving'amuzi pamoja na dishi vinapatikana kwa gharama nafuu kabisa ya Sh.99,000/- kwa mawakala wote wa DStv nchini.
IMG_0443
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi ya begi kwa mwandishi wa habari, Joseph Michael baada ya kuchezesha droo kwa waandishi waliohudhuria mkutano huo. Wanaoshuhudia kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
IMG_0454
Furaha Samalu na Barbara Kambogi wakikabidhi zawadi ya begi Super Sport kwa mpiga picha wa ITV, Abdallah Kaniki aliyeibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa na Multichoice Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
IMG_0458
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi akikabidhi zawadi ya T-shirts kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Imani Makongoro.
IMG_0419
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Msimu mpya wa Soka 2015/16, unatarajia kuanza rasmi Jumapili ijayo kwa kushuhudia ligi mbalimbali Duniani zikichezwa na kurushwa moja kwa moja kupitia SuperSport ambayo imejipanga kukuletea burudani kabambe kwa mashabiki wa soka barani Afrika.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania , Ronald Baraka Shelukindo mapema jana akizungumza na vyombo vya habari amebainisha kuwa, Wateja wa DStv wakae tayari msimu huu kwenye Ulimwengu wa Mabingwa ambapo timu mbalimbali zimejiimalisha katika kuakikisha zinatwaa ubingwa.
“Ligi ya mwaka zitakuwa za kasi na kuvutia kwa kila timu. Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine, huku Manchester United wanahitaji kurudisha kiti chao cha Ubingwa Uingereza. Jose Mourinho analenga kuhakikisha Chelsea inabaki juu, wakati huo huo , Hispania inajiandaa kuhakikisha wanashinda kwa mara ya tatu kombe la Euro 2016.” Ameeleza Baraka Shelukindo.
Ameogeza kuwa, Watazamaji wa SuperSport watakuwa na nafasi ya kipekee kushuhudia mechi kwenye ubora wa HD, ikiwa ni pamoja na michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) , Ligi ya Hispania (La Liga) , Ligi ya Mabingwa wa Ulaya(UEFA) na Ligi ndogo ya Ulaya ( Europa) ,mechi za FIFA za kirafiki za kimataifa na Klabu Bingwa ya Dunia , Kombe la Ujerumani , Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) , Kombe la FA na zaidi.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi anaeleza kuwa, Katika msimu huu , Ulimwengu wa Mabingwa itakuwa ikionyesha mechi zaidi ya 900 za kimataifa. Wateja wa DStv Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi ya 450 ‘live’, huku Wateja wa DStv Premium watazawadiwa mechi zote ‘Live’ zitakazorushwa katika chaneli zote za SuperSport .
“Kuanzia msimu huu na kuendelea, vituko vyote vya Ligi Kuu ya Uingereza vitakuwa vikiletwa kwenu kupitia SuperSport 5 ( SS5 ) inayopatikana kwenye kifurushi cha Premium. SS5 sasa itakuwa ni nyumba ya soka la Afrika kwa ligi kuu ya Uingereza huku ikijumuisha mechi 3 ‘Live’ kila Jumamosi na Jumapili. Kuambatana na mechi kutakuwa na vipindi maalum vya soka kama PLTV Kick Off, Match Day Live, Fan Zone, Saturday/Sunday Review, Football Today, Classic Matches, Netbusters na Mech za Wiki” Amebainisha Barbara Kambogi.
Moto wa La Liga utawashwa ndani ya SuperSport 3 ( SS3 ). Chaneli hii itakuwa inakuletea mechi hadi tatu za ligi ya Hispania ‘ Live’ kwa siku ya Jumamosi na Jumapili . Wateja wa DStv Premium na Compact Plus watapata nafasi ya kuangalia mechi za michuano ya Kombe la mashindano Uingereza ndani ya SS3 sambamba na mechi za Jumamosi mchana za Ligi kuu ya Uingereza , mbadala wa mechi inayorushwa ndani ya SS5, pamoja na Ratiba zote za Jumatatu usiku na vipindi vya mahojiano vya studio.
Pamoja na Mechi za ‘Live’ ndani ya SS3 , itakuwa inakuonyesha vipindi muhimu vya shoo za magazeti , yanayojiri ndani ya La Liga, pamoja na vipindi maalum vya ligi za soka . Makombe yote ya mpira wa miguu, Mabingwa wa Ulaya na Ligi ya Europa, Kombe la FA , Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey), Kombe la Ujerumani , Euro 2016 na mechi za kirafiki za kimataifa zitaendelea kutapatikana kwenye SS3 .
Kwa habari zaidi za michezo na ratiba za mechi kwenye SS5 na SS3, tafadhali tembelea www.supersport.com
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

VITUKO VYA UCHAGUZI:KWELI NJIA YA MUONGO NI FUPI,DUUH..MHINDI ALIYEKAMATWA NA TAKUKURU UKONGA AKANA KUGAWA FEDHA KWA WAPIGA KURA,NIMEKUWEKEA MAELEZO ZAIDI YAPO HAPA

T888DED na T 183 CJQ ni Magari haya ndiyo yaliyohusika katika tukio zima la ugawaji rushwa huo yakiendeshwa na wapambe wa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Ukonga Ramesh Patel pamoja na Prof. Felician Barongo ,Msafiri Mohamed DK, Na wengine walikamatwa na Takukuru juzi usiku katika ukumbi wa check point Pugu wakigawa rushwa kwa wajumbe wa mashina ili kuwahamaisha kumshangilia leo kwenye mkutano wa kuomba kura katika kata ya Pugu na hatimaye kumpigia kura za maoni 1/8/2015.
Ramesh na wapambe wake waliingia na magari mawili aina ya Nissan Extrail moja likimilikiwa na Prof. Barongo na lingine na Msafiri DK Magari haya ndio yanayoongozana na Ramesh toka Jumamosi kwenye kata za mzinga,kitunda,kivule na ukonga.
Baada ya Takukuru kuvamia magari hayo, na kumweka chini ya ulinzi msafiri DK na dereva aliyefahamika kwa jina la Dotto kina Barongo na wenzake walimtoa Ramesh mlango wa nyuma na kupakiwa bodaboda kuondoka eneo la tukio bila dereva wa bodaboda kujua amebeba mjumbe wa NEC na mtuhumiwa wa rushwa!
T 671 BQL aina ya Nissan X-TRAIL NAYO ILIHUSIKAKATIKA TUKIO HILO,hapa linatimua mbio baada ya ishu nzima kubumburuka
Afisa usalama mmoja nae alidandia bodaboda na kuanza kumfukuza. Baada ya mwendesha bodaboda kujua anakimbizwa aliingia kwenye njia isiyotoka na hapo Ndio Ramesh alipotiwa nguvuni.
Mdau wetu alifika eneo la tukio na kuongea na mashuhuda kuthibitisha tukio hili. Pamoja na picha za nyumba hiyo pugu kigogo karibu na Check Point
Katika hali ya kujihami na kujisafisha Ramesh Patel amekana kuhusika katika tukio hilo ingawa ushahidi upo mfano picha hizi hapa chini baada ya kukamatwa siku ya tukkio eneo la check point pugu Dar es Salaam na Maofisa wa TAKUKURU.
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

NAMNA YA KU-DOWNLOAD VIDEO YEYOTE YOUTUBE KWA SIMU AU KOMPYUTA BILA SOFTWARE


Watu wengi watumiaji wa mtandao hukutana na wakati mgumu sana wakitaka kupakua video kupitia kompyuta au simu bila program au software yeyote.

Imezoweleka mara nyingi kutumia Internet Download Manager lakini mara nyingi imakuwa ikidumu kwa siku 30 tu za bure vinginevyo utatakiwa kununua au uipate ambayo imefanyiwa cracking.

Kupitia maelezo haya utaweza kushusha video yeyote kutoka mtandao wa YouTube bila software yeyote ile kwa kufuata njia zifuatazo:
Hakikisha una URL ya video unayoitaka
Ondoa au futa "http(s)//:www." kisha andika "ss" na bofya ENTER, halafu subiri kidogo.

Download: Internet Download Manager with Crack For Free [Software]



chagua ubora wa video uitakayo na uanze kuishusha mara moja huku ukiisubiri kwa hamu.

"Kwakuwa hii ni teknolojia lazima kuna njia nyingine basi usisite kutuandikia kupitia sehemu ya maoni kwa njia ya facebook hapo chini.


Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kashikashi ya Magogo Barabarani Yaleta Hofu

Mmoja wa wahanga wa tukio la kusitisha safari baada ya kuwekwa magogo barabarani akisubiri pawe shwari kabla ya kuendelea na safari yake.
Habari hii imeandikwa na mhariri wa blog ya Keronyingi

ANAELEZA; Alfajiri ya juzi tar 06 Feb, kuamkia jana nikiwa na ndugu zangu tunatokea Tabora kuelekea Dar kwa gari dogo aina Toyota Mark X ghafla tukiingia kijiji cha Bwawani tukakuta msururu wa magari mengi (malori) yakiwa yameegeshwa pembeni mwa barabara baadhi ya watu waliokuwa nje ya malori hayo wakatusimamisha, tulipotaka kujua kulikoni ndipo tukaambiwa kuwa nje kidogo ya kijiji hicho cha Bwawani kuna watu wanaosadikiwa majambazi wametega magogo kwa dhamira ya kuteka magari na kufanya unyanganyi na kuwa tayari walishafanya mawasiliano na Polisi Chalinze kuwapa taarifa hiyo hivyo nasi tukaegesha pembeni na kuanza kusubiri.

Baada ya kama nusu saa hivi ya kutoona gari la aina yeyote kupita tokea Chalinze tukathibitisha ni kweli paliwekwa magogo. Baada ya dakika 40 hivi baadhi ya malori yakaanza kuondoka kuelekea Chalinze huku wakituambia majambazi hao wameshaondoka, lakini hata hivyo tukasita kuyafuata yale malori mpaka ikatokea Toyota Noah toka Chalinze ndipo sisi na wenye magari mengine tukaanza tena safari ya kuelekea Dar.

Kilichoshangaza ni kutokuwa na kauli rasmi toka Polisi Chalinze kuthibitisha ni kweli majambazi wale walishaondoka eneo walilotega magogo. Zaidi ni matumaini yangu na wadau wengine kuwa serikali itaimarisha doria eneo hilo ambalo limetajwa kutumika mara kwa mara na majambazi hao.
Subira yavuta kheri
Gari nililokua nikiendesha toka Tabora
Malori yakiwa yameegeshwa pembeni
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Taarifa ya StarTimes Dhidi ya EATV na ITV


Leo mchana starmedia Tanzania iliitisha mkutano na waandishi wa habari kuzunguzia mambo mbalimbali sanasana kuhusu suala la ITV na EATV na sio kama ilivyotengenezwa na watu wa ITV. Mkutano huu ulihudhuriwa na waandishi mbalimbali wakiwemo ITV, STARTV, CHANEL TEN, TV1, CLAUD, SIBUKA, na vyombo vingine vya habari.
Pia mkutano huu ulihudhuriwa na wataalamu wa masafa kutoka TCRA. Taarifa hiyo ilikuwa kama ifuatavyo’

Taarifa kutoka kwa wataalamu wa STARTIMES 

ITV na EATV zimekuwa zikionekana vibaya kwa watumiaji wa ving’amuzi vya STARTIMES kuanzia tarehe 27 january 2015, hali hii imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa sana kwa wateja wetu na umma kwa ujumla ambao wamekuwa wakifurahia chanel hizi katika vingamuzi vyetu. Wataalamu wetu walijaribu kufuatilia kwa ukaribu kujua tatizo katika mitambo yetu na wakagundua kwamba kulikuwa kuna mwingiliano wa mawimbi kutoka chanzo cha nje ‘WiMAX Operator’, hali hii ilitufanya sisi kama startimes kuwasiliana na mamlaka ya mawasiliano TCRA, kwani wao ndio wasimamizi wakuu wa masafa mbalimbali. Kuanzia tarehe hapo timu ya wataalamu kutoka STARTIMES na TCRA wamekuwa wakifanya kazi ya uchunguzi kujua ni ‘WiMAX operator’ gani ambaye amekuwa anasababisha hali hiyo. Katika uchunguzi uliofanywa na TCRA na STARTIMES ikagundulika yafuatayo
  1. Kuna ‘WIMAX Operator’ mpya ambaye amekuwa akisababisha muingiliano huu katika dishi la STARTIMES linalopokea mawimbi ya ITV na EATV makongo 
  2. ‘operator huyu amekuwa akirusha mawimbi yake katika masafa yenye ukubwa wa 3.598MHZ. Masafa haya yanakaribiana sana na masafa ya ITV/EATV dishi ambayo ni 3.644 na hivyo kusababisha muingiliano wa mawimbi hasa wakati wa jioni 
  3. Nguvu ya mawimbi anayorusha ‘WIMAX operator’ huyu ni kubwa ukilinganisha na mawimbi tunayopokea katika kituo cha makongo 
TCRA nao walizungumza kama ifuatavyo Tatizo la ITV na EATV katika vingamuzi vya STARTIMES limekuwa likisababishwa na muingiliano wa mawimbi na tayari tumegundua kuna ‘WiMAX Operator’. TCRA toka wiki lililopita tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu sana na STARTIMES kuweza kujua chanzo cha tatizo na kutatua tatizo

HITIMISHO
Tunaamini kwamba kutokana na taarifa iliyotolewa na wataalamu wetu na wataalamu wa TCRA ni ukweli kwamba tatizo hili halijasababishwa na STARTIMES kama ilivyoelezwa awali na ITV katika taarifa zao za Habari. Mara zote startimes imekuwa ikifanya kila liwezekanalo kuhakikisha watanzania wanapata chanel zote za nyumbani Hivyo basi tumesikitishwa na taarifa zilizotolewa ITV na ambazo hazikuwa na uchunguzi wowote toka pande husika na kusababisha usumbufu kwa wateja wtu.

Starmedia Tanzania
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mfereji Mpya wa Maji Wahatarisha Watumia Barabara ya Boma Tabora!

Kushoto unaonekana mfereji wa maji. 
Baada ya mfereji huo kuchimbwa na kujengewa kwa mawe, udongo uliotokana na uchimbaji wa mfereji huo umeachwa kando kando ya Boma Road nje ya Holiday Park Guest house na kusababisha adha katika upishanaji wa magari hasa makubwa yapitayo katika barabara hiyo ambayo kabla ya kuachwa vifusi hivyo vya udongo tayari ni nyembamba. Haikuweza kufahamika mara moja ni nani muhusika na huo mfereji lakini huenda ikawa mfereji huo ukawihusu Manispaa ya mkoa wa Tabora. Blogu hii ingependa kuwakumbusha wahusika kuondosha vifusi hivyo ili kuepusha ajali zinazoweza kuotoa eneo hilo.
Barabara ya Boma inavyoonekana pichani 

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Breaking News: Francis Cheka Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Mitatu Jela

Bondia mashuhuri nchini muda mfupi uliopita amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Hiyo ina maana kuwa Cheka anaenda kutumikia kifungo hicho na kutakiwa kulipa fidia ya shilingi millioni 1 kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi meneja wa baa yake iliyopo huko Morogoro
Hukumu hiyo imetokana na kosa la bondia hiyo kumpiga meneja wake aitwaye Bahati kwenye bar ya vijana social mjini Morogoro July 2 mwaka jana alipoenda kudai fedha zake.
Meneja huyo alilazwa hospitali kufuatia tukio hilo ambapo Cheka alidaiwa kumpiga ngumi. Katika kesi hiyo Cheka alikuwa anakana mashtaka.

Bondia huyo anaenda jela huku akiwa anashikilia mkanda wa dunia wa WBF Super Middleweight.

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

"Muziki Si Lolote Kwa Msanii Asiyewekeza Fedha" Said Fella


Mwanzilishi wa kundi la muziki Wanaume Family na Yamoto Band, Said Fella amesema kama msanii anataka kufanya muziki, lazima yeye au uongozi unaomsimamia wawekeze fedha kwenye muziki wake.

Fella amewataka wasanii kuacha kuupeleka muziki wao kishkaji shkaji na waonyeshe nia ya dhati kwenye muziki wao.
“Kila msanii ana malengo na muziki anaoufanya, ukiamua kuwa mwanamuziki kampuni lazima utie pesa’, yaani uamue kabisa ngoja nifanye muziki fulani. Maana ya pesa sio lazima uwe na milioni kumi, milioni ishirini. Ni useme ‘mimi sitaki mwana Marco Chali anitengenezee beat bure au Adam Juma anifanyie video bure kishkaji shikaji tu. Yaani Adam Juma akisema milioni nne mpe milioni nne akufanyie kazi yako. Marco Chali akisema beat laki tano mpe laki tano yake afanye kazi yake. Mpaka hapo ndo tutakuwa tumejiweza kufanya biashara ya muziki, kufanya muziki ule wa kampuni,” amesema Fella.
“Kikubwa kila msanii anatakiwa kuwa na nia na achokifanya,” ameongeza. “Kwa sababu mwisho wa siku kila msanii anatakiwa kutambua anafanya muziki gani? Huu muziki ninaofanya ni wa biashara au la? Au muziki wa maendeleo. Ukifanya muziki wa kikampuni ina maana sitaki tena nidondoke. Kwahiyo lazima utakuwa unatengeneza muziki wako pamoja na maisha yako.”
“Lakini kuna watu wengine wanafanya muziki lakini hawana malengo kama hayo niliyoyasema, wana malengo mengine wanayoyafikiria. Wengine wanasema nikipata pesa ninunue gani, wengine ninunue nyumba kila mmoja ana malengo yake. Kwahiyo lazima ujitambue muziki gani unataka kufanya.
Hata mimi sikumwambia Master Jay kwamba muziki anaoufanya Shaa ni mbaya, ila nilimwambia kuna muziki akifanya Shaa mafanikio yatakuwepo, kwamba huyu anafanya ndiyo lakini wanasikiliza matajiri lakini tajiri atasikiliza muziki wakati yupo kwenye gari, atasikiliza muziki kama ataenda kwenye kumbi za starehe. Lakini akiwa ofisini kwake ataangalia muziki wa Ulaya tu, hafikirii muda wote kwamba atasikiliza muziki wa fulani. Lakini kuna watu wanasikiliza muziki huo muda wote na ndo kama maisha yao. Ndio maana Shaa akaamua kufanya muziki unaopendwa na watu wengi.”
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

UPDATES: Baraza Jipya la Mawaziri Tanzania

Ikulu imeitisha mkutano wa ghafla na waandishi wa habari muda huu na mkutano huo utaanza ndani ya nusu saa kuanzia sasa. Taarifa zinasema ni kwamba mkutano huu umeitishwa ili kutangaza mabadiliko madogo ya mawaziri na mawaziri hawa wanapaswa kuapishwa kesho kabla ya Rais Kikwete kuondoka kwenda Davos Uswisi kesho hiyo hiyo jioni.
Tutakujuza kinachoendelea Ikulu

UPDATES:

Katibu Mkuu kiongozi anasoma majina ya mawaziri walio teuliwa
1. George Simbachawene- Waziri Nishati
2.Mary Nagu-Waziri wa Nchi mawasiliano na Uratibu
3.Christopher Chiza-Waziri uwezeshaji na Uwekezaji
4.Halson Mwakyembe-Ushirikiano wa afrika mashariki
5.Lukuvi-Ardhi Nyumba na Makazi
6.Steven Wasira-Kilimo chakula na Ushirika
7.Samwel Sitta -Wizara ya Uchukuzi
8.Jenista Muhagama-Sera na uratibu wa Bunge

Mawaziri Kamili
George Simbachawene- Waziri wa Nishati na Madini
Mary Nagu -Waziri wa nchi Mahusiano na Uratibu
Harrison Mwakyembe - Waziri wa Afrika Mashariki.
Wiliam Lukuvi - Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
Steven Wassira - Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
Samwel Sitta - Waziri wa Uchukuzi
Jenista Mhagama - Waziri wa Sera na Uratibu wa Bunge
Christopher Chiza- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji

Manaibu Waziri
Steven Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
Angellah Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi
Ummy Mwalimu- Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Anna Kilango- Naibu waziri wa Elimu
Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

Tutaendelea kuwajuza

Credit: TheChoice
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MAREKANI NA UJERUMANI WAIPA TANZANIA VIFAA VYA KUKABILIANA NA UJANGILI MBUGA YA SELOUS

Meneja wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous leo
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

WAFANYABIASHARA MBEYA, WAANDAMANA MAHAKAMANI

Wafanyabiashara wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masoko zaidi ya matano yaliyopo Jijini Mbeya, wakiwa nje ya mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru, Mwenyekiti wa Soko la Soweto Honola Mbogella ambaye alifikishwa mahakamani hapo na halmashauri ya jiji la Mbeya kwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.

MWENYEKITI wa Soko la Sowetojijini Mbeya, Honola Mbogella, amefikishwakatika mahakama ya Mwanzo Mbeya mjinikwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.


Kufuatia kukamatwa kwaMwenyekiti huyo kulisababisha zaidi yawafanyabiashara 1000 wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masokomatano yaliyopo Jijini Mbeya, kuandamana na kuizunguka mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru.


Mwenyekiti huyo,amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, leo na kesi yake kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi ambapo kesi hiyo ilivuta hisia za watukutokana na kundi hilo la wafanyabiashara kuizunguka mahakama hiyo, huku jeshila polisi likilazimika kuimarisha ulinzi.


Akisomewa mashitaka hayo Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Mbeya MjiniUbaswege Mathew, karani wa Mahakama hiyo, Sioni Kasunga, alisema mtuhumiwa huyoalifanya kosa hilo January 10 mwaka huu akiwa katika eneo lake la kazi la Sokola
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema, kwa mujibu wa kifungu kidogocha cha sheria namba 101(a) sura ya 288iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wahalmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.


Alisema, mtuhumiwa aliwazuiawafanyabiashara hao kugoma kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi 300 na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa maelezokwamba licha ya wafanyabiashara hao kulipiatozo hiyo kwa kipindi kirefu bado soko hilo limeendelea kukithiri kwa uchafu.


Aidha, kutokana na kosa hilo,Hakimu wa mahakama hiyo, Ubaswege Mathew,baada ya kusikiliza maelezo hayo,alitoanafasi kwa mtuhumiwa ambaye alikana shitaka hilo hivyo, hakimu kuhairisha kesi hiyo mpaka kesho na kwamba dhamana kwa mtuhumiwa ipo wazi.


“Kesi hii nimeihairisha mpaka kesho asubuhi, mtuhumiwa anahaki ya kuwekewadhamana kwa masharti ya kiasi cha fedha cha shilingi milioni mbili na wadhaminiwawili mmoja akiwa ni mtumishi wa
serikali,”alisema Wakati kesi hiyo ikiendeleamahakamani hapo, umati mkubwa wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zaokatika masoko matano ya Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na Uhindiniulijitokeza na kuizunguka mahakama hiyo kwa kile walichokidai kwamba Mwenyekityi huyo ameonewa. 


Wakizungumza naMbeya yetu ,nje ya mahakama, wafanyabiashara hao ambao waligoma kutaja majina yao, walisemawao wamegoma kulipa ushuru huo kutokana na halmashauri kushindwa kuetekelezamajukumu yao ya ukarabati wa miundombinu pamoja na usafi wa mazingira hivyoMwenyekiti huyo hausiki na suala lakuwashawishi kugoma kama inavyodaiwa na halmashauri.


Hata hivyo, wafanyabiashara haowamegoma kuendelea na shughuli zao mpaka suala hilo litakapo patiwa ufumbuzikwa halmashauri kurekebisha miundombinu na usafi wa mazingira katika maeneo yabiashara.
Mwisho. 
Na Mbeya yetu
Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
© Copyright Mahaba Live
Back To Top