Featured
Loading...

WAFANYABIASHARA MBEYA, WAANDAMANA MAHAKAMANI

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


Wafanyabiashara wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masoko zaidi ya matano yaliyopo Jijini Mbeya, wakiwa nje ya mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru, Mwenyekiti wa Soko la Soweto Honola Mbogella ambaye alifikishwa mahakamani hapo na halmashauri ya jiji la Mbeya kwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.

MWENYEKITI wa Soko la Sowetojijini Mbeya, Honola Mbogella, amefikishwakatika mahakama ya Mwanzo Mbeya mjinikwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao.


Kufuatia kukamatwa kwaMwenyekiti huyo kulisababisha zaidi yawafanyabiashara 1000 wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masokomatano yaliyopo Jijini Mbeya, kuandamana na kuizunguka mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru.


Mwenyekiti huyo,amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo yaMbeya mjini, leo na kesi yake kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi ambapo kesi hiyo ilivuta hisia za watukutokana na kundi hilo la wafanyabiashara kuizunguka mahakama hiyo, huku jeshila polisi likilazimika kuimarisha ulinzi.


Akisomewa mashitaka hayo Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ya Mbeya MjiniUbaswege Mathew, karani wa Mahakama hiyo, Sioni Kasunga, alisema mtuhumiwa huyoalifanya kosa hilo January 10 mwaka huu akiwa katika eneo lake la kazi la Sokola
Soweto lililopo Jijini Mbeya. Alisema, kwa mujibu wa kifungu kidogocha cha sheria namba 101(a) sura ya 288iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mtuhumiwa aliwazuia watumishi wa umma wahalmashauri ya Jiji la Mbeya kufanya kazi yao ya kukusanya ushuru.


Alisema, mtuhumiwa aliwazuiawafanyabiashara hao kugoma kutozwaushuru wa shilingi 200 hadi 300 na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa maelezokwamba licha ya wafanyabiashara hao kulipiatozo hiyo kwa kipindi kirefu bado soko hilo limeendelea kukithiri kwa uchafu.


Aidha, kutokana na kosa hilo,Hakimu wa mahakama hiyo, Ubaswege Mathew,baada ya kusikiliza maelezo hayo,alitoanafasi kwa mtuhumiwa ambaye alikana shitaka hilo hivyo, hakimu kuhairisha kesi hiyo mpaka kesho na kwamba dhamana kwa mtuhumiwa ipo wazi.


“Kesi hii nimeihairisha mpaka kesho asubuhi, mtuhumiwa anahaki ya kuwekewadhamana kwa masharti ya kiasi cha fedha cha shilingi milioni mbili na wadhaminiwawili mmoja akiwa ni mtumishi wa
serikali,”alisema Wakati kesi hiyo ikiendeleamahakamani hapo, umati mkubwa wa wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zaokatika masoko matano ya Soweto,Uyole, Mabatini, Sokomatola na Uhindiniulijitokeza na kuizunguka mahakama hiyo kwa kile walichokidai kwamba Mwenyekityi huyo ameonewa. 


Wakizungumza naMbeya yetu ,nje ya mahakama, wafanyabiashara hao ambao waligoma kutaja majina yao, walisemawao wamegoma kulipa ushuru huo kutokana na halmashauri kushindwa kuetekelezamajukumu yao ya ukarabati wa miundombinu pamoja na usafi wa mazingira hivyoMwenyekiti huyo hausiki na suala lakuwashawishi kugoma kama inavyodaiwa na halmashauri.


Hata hivyo, wafanyabiashara haowamegoma kuendelea na shughuli zao mpaka suala hilo litakapo patiwa ufumbuzikwa halmashauri kurekebisha miundombinu na usafi wa mazingira katika maeneo yabiashara.
Mwisho. 
Na Mbeya yetu

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top