Bw. TIMANYWA akisisitiza jambo kwenye ufungaji wa mafuzo hayo baada ya kupewa zawadi.
Kamanda MISIME akikabidhi vyeti vya mafunzo kwa washiriki.
Kamanda MISIME akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi toka Jeshi la Polisi.
Kamanda MISIME kiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa shirika la APEC.
Kamanda wa Mkowa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP akikabidhiwa zawadi na waendesha pikipiki (Bodaboda).
Mkurugenzi Mtendaji wa APEC Bw. RESPICIUS TIMANYWA akiongea jambio kwenye ufungaji wa mafunzo hayo.
RPC Dodoma DAVID MISIME akiongea katika ufungaji wa mafuzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza kwa mkini.
Washiriki wa mfunzo hayo.
Na. Sylvester Onesmo wa
Jeshi la Polisi Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na wadau wengine litaendeleza msako kwa wale wote waendesha pikipiki ambao hawana leseni kwani walishapewa muda mrefu ili waweze kupata leseni pamoja na mafunzo ya udereva.
Ameyasema hayo wakati wa kufunga mafuzo kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) wa Manispaa ya Dodoma yaliyoendesha na Shirika lisilo la kiserikali la –APEC - kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mafunzo yaliyochukua wiki moja kuanzia tarehe 12/01/2015 hadi tarehe 19/01/2015.
Kamanda MISIME amesema elimu walioipata waendesha pikipiki (bodaboda) waitumie vizuri ili kujiepusha na ajali ambazo kwa kiwango kikubwa zinasababishwa na makosa ya kibinadamu na ukosefu wa mafunzo.
Aidha Kamanda MISIME ameeleza kuwa takwimu za kuanzia mwezi Januari hadi Desemba 2014 zinaonyesha ajali za pikipiki zilikiwa 62, kati ya hizo ajali za vifo ni 16 ambazo zilisababisha vifo vya watu 18. Pia ajali za majeruhi zilikua 28 na jumla ya watu 31 walipata majeraha sehemumbalimbali. BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI
















