Kupitia ukrasa wake wa Facebook, nguli wa TAKEU style na muziki Tanzania Mr Nice amefunguka na kulalamikia gazeti la Mwananchi ambalo limechapisha habari anazo kanusha na kusema si kweli bali wanamchafua. Mr Nice amefunguka kama ifuatavyo:
--------
"Gazeti la mwananchi mmenikosea heshma sana kwa kuniandika habari za uongo..sijui mmezitoa wapi na kwa uhakika upi....mimi sisumbuliwi na maradhi ya aina yoyote yale....nimewakosea nini mpaka muandike story kama hii..?????? je huku ndiko mnakowaambiaga wananchi na mashabiki wetu kuwa mnatusaidia kuwajulisha habari wapenzi na mashabiki wetu kwa story za kujitungia kama hii...??????? Hapa msaada wenu kwangu ktk story hii ya uongo kwa mashabiki wangu ikowapi sasa...!!!?
Jamani sii wasanii wote wanapenda kuandikwa magazetini hovyo kwa story za kutunga ili kujitafutia umaarufu plz,wengine tunajijua sana umaarufu wetu ni wa kiwango kipi na tuutumieje na si kwa story za uongo gazetini kila siku...eti sionekani!!! Ina maana mtu asipoonekana akaamua kukaa na kupumzika nyumbani kwake bola kuzurura hovyo tayari anakuwa mgonjwa aliyetetereka..? Nilishakuja hapo ofisini kwenu kuchukua dozi za ugonjwa wowote labda au!!!
Mpaka muwe na ujasiri wa kuniandika kuwa mi ni mgonjwa nimetetreka ndiyo maana sionekani.!!!!??? Kwa hii story ya leo napenda kuwaambia gazeti la mwananchi mmenikosea sana na nimesikitika sana kuisoma habari maanna inachukiza kwa uongo mliouandika juu yangu..nyie mmeuza gazeti lenu na mmepata pesa kupitia habari hii kwa upande wa mashabiki wangu coz wametaka kununua ili wapate habari juu ya hili mliloandika, ila wakati mnakusanya hela yao mmesahau kuwa mmeniachia wakati mgumu na masononeko mazito moyoni mwangu na mashabiki wangu pia...mimi ni binadam na nina moyo kwa wenu wala sina moyo wa plastic napenda kuwaambia gazeti la mwananchi story hii sijaipenda na imenisononesha sana kunizushia maradhi wakati mi ni mzima....leo mmeamua kuzusha mr nice ametetreka kwa maradhi,kesho mtasema kabisa mr nice amekufa........EEEEE MUNGU WASAMEHE ILA UWATANGULIZE WAO KTK HAYO WANAYONIOMBEA..thnks
KATIKA POST NYINGINE ALIANDIKA HIVI PIA
--------
"Mwandishi wa habari hii ni mpumbavu namba moja tena ingekuwa vizuri hao waliomujiri wapime uwezo wake wa kuwapelekea habari,maana hii ni habari ya ki~~nge sana juu yangu..mi ni mzima wa afya na sina hata homa ya makamasi wachilia mbali ukimwi na ebola,iweje gazeti hili litafute cha kujazia kwenye page zake ikikosa itunge story za uongo na kuzichapisha gazetini..!!?
Eti afya ya mr nice imetetereka???? "Fuck them idiot "... siumwi homa yoyote hata ya manjano we mwandishi poyoyo ulieandika habari hii, umezoea kuona wasanii wanazagaa hovyo hovyo huko mitaani basi unachukulia wote tuko hivyo...ninajijua na ninajitambua sana kuwa mi ni nani na ndo maana napenda kujiheshimu na ndicho kitu ambacho mashabiki na familia yangu wanakijua juu yangu...mimi siumwi ugonjwa wa aina yoyote ni mzima wa afya na roho,na hata majeraha niliyopata ktk ajali nimeshapona sasa hii story ya mimi kusumbuliwa na maradhi umeitoa wapi wewe na una ushahidi gani hadi kufikia hatua ya kuniandika gazetini kwako eti nimetetereka....gazeti lako halifanani na story hii au labda unapiga deiwaka hapo maana story hizi utazikuta kwenye magazeti ya udaku na si hili....usiwadanganye mashabiki wangu wala watanzania kwa kunizushia uongo plz....sijapenda story ya gazeti lako juu yangu maana ni ya uongo tena ya kutunga.."
--------
PIA ALIONGEZA:
Katika moja ya mirejesho yake katika maoni aliona kuwa;
"Kwa kweli sasa kuna haja ya kuwa na wanasheria binafsi wa kupambana na ujinga kama huu dada yangu,wao wanaingiza pesa kwa kutumia jina la mtu then wanauacha katika lindi kubwa la matatizo bila wao kujali maumivu yake...kesho wanasema gazeti hili liko mbele kuwapromote wasanii..je kuzushiana magonjwa ndiyo kumpromote msanii ktk gazeti hili liitwalo MWANANCHI..??????? siyo poa namna hii"







