Featured
Loading...

Happy Birthday Sheddy Clever

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


Pro. Sheddy Clever

Hii ni siku ya pekee kwa muandaaji (Producer) wa Kitanzania ambaye katika mafanikio makuwa ya uandaaji wa kazi zake za muziki wa Kitanzania ameinuka kuwa NURU kubwa ya kuigwa na vijana wengi hasa pale alipoifanya kazi ya My Number One ya msanii mkubwa nchini na nje Diamond Platinumz (Nasbu Abdull). Kazi hiyo imeweza kuingia katika orodha ya tuzo nyingi kama vile AFRIMMA, BET na nyingine za nchini kama Kili Music Awards. Pia amezalisha kazi nyingi kama Msambinungwa ya Tunda Man, Zilipendwa ya Matonya, Merry Me ya Rich Mavoko, Kerewa ya Shetta na nyingine nyingi.

Pia producer huyu alifanikiwa kuingia katika tuzo za AFRIMMA hata Kili Music Awards pia katika mwaka huu wa 2014. Producer Sheddy Clever bila shaka hataujutia mwaka huu kwa namna ya pekee kadri ya kipaji chake kilivyovuma na kung'ara nchi nzima na kwingineko duniani.


Ni hakika pia amekuwa moja wa mfano wa kuigwa sana na vijana waishio na vipaji vyao huku wakiwa na hitaji kubwa la mafanikio.

MUNGU AMZIDISHIE MEMA NA FADHILA NYINGI KIJANA HUYU KATIKA SIKU YAKE MUHIMU HAPA DUNIANI NA AWEZA KUYAKABILI YOTE KWA UWEZA NA MAJALIWA YA ALIYEMLETA HAPA DUNIANI IKIWA NI PAMOJA NA WAZAZI NA WALEZI WALIOMKUZA KWA MAADILI.

HAPPY BIRTHDAY SHEDDY CLEVER


Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top