Featured
Loading...

UOKOAJI: Updates: Airasia QZ8501 Miili Yaanza Kuwasili Nchini Indonesia

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


Wanajeshi wakiwa wamebeba miili ya mwanzo ya watu waliokufa katika Ndege ya AirAsia.

MIILI ya mwanzo ya watu wawili waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia QZ8501 imewasili leo jijini Surabaya, Indonesia ambapo ndugu na jamaa wanasubiri kwa utambuzi.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200, ilipotea Jumapili iliyopita ikiwa imebeba watu 162 ikitokea Surabaya kwenda Singapore, ambapo baadhi ya miili imeanza kupatikana jana katika Bahari ya Java.

Watu 155 kati ya 162 waliokuwa katika ndege hiyo ni raia wa Indonesia.
Baadhi ya mabaki ya Ndege ya AirAsia yakiwa Uwanja wa Ndege wa Pangkalan Bun, Indonesia leo.
Mwili wa mmoja wa watu waliokuwa kwenye ndege ya AirAsia ukielea katika Bahari ya Java.
Maofisa wa Kikosi cha Uokoaji wakiichunguza ramani inayoonyesha eneo ilipokutwa miili ya watu waliokuwa katika AirAsia.
Ndugu na jamaa wa watu waliokuwa kwenye Ndege ya AirAsia wakiwa na simanzi baada ya kupata taarifa za kupatikana kwa miili baharini.

JITIHADA za kuopoa miili kutoka katika Ndege ya AirAsia QZ8501 iliyoanguka baharini Jumapili iliyopita ikiwa na watu 162 zimeendelea kukwamishwa na hali mbaya ya hewa.

Ndege hiyo ilianguka katika Bahari ya Java nchini Indonesia na hali ya dhoruba katika eneo la uokoaji imezidi kukwamisha zoezi hilo.

Mamlaka nchini Indonesia yamethibisha kuwa mabaki yaliyoonekana majini eneo la Borneo ni ya ndege iliyopotea ya AirAsia.

Rais wa Indonesia, Joko Widodo, ameahidi kuendelea kufanya uchunguzi wa kina kwa kutumia meli na helkopta kuhakikisha miili ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo inapatikana.

Maombolezo ya pamoja yanatarajiwa kufanyika leo huko Surabaya nchini Indonesia na Gavana wa Jimbo la Java Mashariki, Soekarwo ameeleza kuwa sherehe zote za Mwaka Mpya zimesitishwa kutokana na ajali hiyo ya AirAsia.

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top