Featured
Loading...

WANNE WAFA WAKIHOFIA KUTOKEA AJALI HUKO PWANI

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE




WATU wanne wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Abiria la Hajees likitokea Tanga kwenda Dar es Salaam na lori katika eneo la Mandera Mkoani Pwani leo asubuhi.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrich Matei amesema kuwa abiria hao waliruka kutoka katika basi hilo kuhofia ajali ya kugongana na lori lililokuwa likitokea mbele ya basi hilo na ndipo walipoangukia barabarani na kupelekea vifo vyao, baada ya dereva wa basi kutoka nje ya barabara.

Aidha Kamanda Matei amesema kuwa katika uchunguzi wa awali wa Chanzo cha ajali hiyo wanamshikilia dereva wa lori hilo ambalo lilisababisha vifo vya abiria hao walioruka kutoka katika basi la Hajees. [Source: GLP]

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top