Featured
Loading...

Story Kuhusu Kikundi cha ‘Panya Road’ Kuvamia Maeneo Mbalimbali Dar…

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


katika hali isiyo ya Kawaida na ya kuogopesha, kumeibuka taharuki kubwa usiku huu kwa Wakazi wa maeneo mbalimabali ya jiji la Dar, ikiwemo, Sinza, Kinondoni, Mwananyamala, Mabibo, Magomeni, Manzese, Kagera na Mburahati kwa kile kinachoelezwa kuwa vijana waitwao Panya Road wamevamia maeneo hayo na kuwajeruhi watu kwa vitu vyenye ncha kali,visu na mapanga na kuwapora vitu (mali zao) walivyokuwa navyo,kama vile haitoshi baadhi yao wamevunjiwa vioo vya magari yao.

Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa vijana hao waitwao Panya Road wameibuka na kufanya uhalifu huo mara baada ya tukio la Mwenzao mmoja kudaiwa kuuwawa na Polisi.



Aidha Chanzo hicho kimebainisha kuwa baada ya taarifa kusambaa kwa haraka,kimeeleza kuwa Jeshi la Polisi limeingia kazini kuwasaka watuhumiwa hao walioibua tafrani kubwa usiku huu. 

Wadau tutazidi kuwaletea taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kadiri ya zitakavyokuwa zikipatikana.

Via Michuzi Blog

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top