Na Magreth Magosso,Kigoma.
IMEFAHAMIKA kuwa,Mradi wa Mtandao wa maji unaojengwa katika Manispaa ya Kigoma Ujiji huenda usiwe na tija kwa wananchi wa hapo,endapo serikali haitawapa fidia ya fedha mapema kaya zitakazoathiriwa na mradi huo.
Mradi umetengewa sh. Bilioni 32 ,kwa ufadhili wa jumuiya ya ulaya,serikali ya ujerumani (KFW)na serikali ya nchi hii, katika ujenzi wa matanki ya maji eneo la vamia,mlole,gungu,mji mwema,mnarani,kigoma sekondari sambamba na usambazaji wa mabomba makuu kwa urefu wa km16.9 na ya usambazaji maji km 122.8 .
Akifafanua hilo kwenye madhimisho ya kilele cha wiki ya maji kigoma ujiji,Mkurugenzi wa KUWASA Josephat Rwegasira alisema serikali ikiondoa changamoto ya fidia kwa wahanga wa mradi mapema kwa lengo la mkandarasi afanye kazi kwa wakati ,ili ifikapo machi ,17,2015 akabidhi mradi kwa wahusika kwa mujibu wa mkataba wa mkandarasi ‘Specon service Ltd .
Kwa upande wa Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa kigoma Eng.John Ndunguru alisema pamoja na hilo mamlaka inawajibu wa kutoa huduma bora kwa wadau wake ili kuondoa dhulma dhidi ya wananchi husika.
Madiwani ,wananchi wanadai huduma mbovu ya maji na mnawatoza sh.20,000 kwa mwezi, maji kutoka mara mbili kwa mwezi dhulma zaidi hawana kisoma maji(meter)sasa mwishoni mwa machi nisisikie kaya hazina mita, alibainisha Eng.Ndunguru.
Aliongeza kwa kusema kuwa, amegundua KUWASA haishirikishi vya kutosha wandishi wa habari ,hali inayochangia jamii kukosa taarifa muhimu, kutoka kwa mamlaka sanjari na mikakati yao ili kuondoa dhana hasi kwa wadau dhidi yao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi wa kigoma ujiji Mariamu Issa na Sophia Steven walisema , madhimisho ya wiki ya maji haina tija, kutokana na adha ya upatikanaji wa maji na kuishauri mamlaka kuwa madhimisho yawe wazi ili kubaini changamoto baina yao.