Featured
Loading...

SEMINA YA MAWAKALA REDD'S MISS TANZANIA 2014

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


Meneja wa bia ya Redd's Victoria Kimaro akisisitiza jambo katika semina ya mawakala wa Redd's Miss Tanzania kulia ni Mkurugenzi wa Lino Hashimu Lundenga na kushoto ni Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria. 
Mawakala wa Redd's Miss Tanzania wakimsikiliza menaja wa bia ya Redd's Victoria Kimaro katika semina ya Mawakala inayoendelea jijini Dar es salaam.
Mwandaaji wa Redd's Miss Simiyu Omari Bakari masamaki katikati akiwa na waandaaji wenzake katika semina ya Mawakala inayoendelea jijini Dar es salaam.
Mwandaaji wa Redd's Miss Tabata akiwa na mwandaaji mwenzake wa Redd's Miss Kigamboni Somoe Ng'itu katika semina ya Mawakala jijini Dar es salaam.
Mwandaaji wa Redd's Miss Pwani Khadija Kalili akiwa amepozi katika semina ya Mawakala wa Redd's Miss Tanzania 2014 jijini Dar es salaam.
Mwandaaji wa Redd's Miss Msasani 2014 ambaye pia ni Mmiliki wa Blog hii, Shabani Tolle akifulaiya jambo na katibu mkuu wa kamati ya Miss Tanzani Bosco Majaliwa katika semina ya Mawakala jijini Dar es salaam.
Mwandaaji wa Redd's Miss Msasani 2014 ambaye pia ni Mmiliki wa Blog hii, Shabani Tolle akiwa na Mwandaaji wa Redd's Miss Tabata 2014 Fred Ogoti.
Meneja wa Bia ya Redd's Victoria Kimaro, akiwa na baadhi ya Mawakala wa Redd's Miss Tanzania 2014 wa kwanza kutoka kushoto Flora Lauwo mwandaaji wa kanda ya Ziwa wa pili kushoto mwaandaaji wa Redd's Miss Msasani 2014 Shabani Tolle ambaye ndio Mkurugenzi wa Blog hii na Fred Ogoti mwandaaji wa Redd's Miss Tabata.
Mwandaaji wa Redd'd Miss Tabora Mkala Fundikira kushoto, mwandaaji wa Redd's Miss Mbeya Amani Mbilo katikati wakijadili jambo na afisa habari wa kamati ya Redd's Miss Tanzania Aidani Ricco wakiwa katika semina ya mawakala inayo endelea jijini Dar es salaam. 
Redd’s Miss Tz 2013 Happines Watimanya akiwa katika picha ya pamoja na mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania 2013 kwenye semina ya mawakala hao kulia waliokaa ni meneja wa Redd’s Original Victoria kimaro na kushoto ni Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria mwenye miwani na wa mwisho ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert makoye.
Meneja wa kinywaji cha Redd’s Origina Victoria kimaro katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa viongozi wa kamati ya Miss Tanzania katika siku ya kufunga semina ya mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania kwa mwaka huu, kushoto kwake ni mkurugenzi wa kampuni ya LINO Intenational Agency Hashim Lundenga, Redd’s Miss Tz 2013 Happines Watimanya na Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria kulia mwenye miwani.
PICHA ZA SEMINA SIKU YA KWANZA HIZO HAPO CHINI
Mawakala wa Redd's Miss Tanzania 2014 wakimsikiliza kwa makini mkurugenzi wa Lino Bw Hashimu Lundenga hayupo pichani katika semina yao ya kuwanoa ambayo inaendelea jijini Dar es salaam.

Na Mwandishi Wetu

MAWAKALA wa mashindano ya urembo nchini wametakiwa kutafuta washiriki wenye vigezo kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo mwaka huu na hatimaye kupata mshindi wa kitaifa “Redd’s Miss Tanzania 2014” atakayeipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye fainali za dunia. 

Akizungumza katika semina ya mawakala hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Regency iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Lino Agency International, Hashim Lundenga(Pichani juu kulia), aliwataka kusaka washiriki bila ya kuwanyanyapaa wasichana kutokana na maumbile yao. 

Lundenga alisema kuwa mawakala hawapaswi kutoa maamuzi ya washiriki wakati wa mchakato wa kutafuta warembo na jukumu la kufanya hivyo litabaki kwa majaji. 

Mkurugenzi huyo alisema pia mawakala wanaume wanatakiwa kuwa makini katika mchakato huo wa awali na kuhakikisha wanaendeleza maadili ya Kitanzania na kufanikisha sanaa hiyo inazidi kufanikiwa. 

“Si vizuri kuwakataa wasichana wanaotaka kushiriki kwa sababu eti wafupi au sabau nyingine…kufanya hivyo si sahihi, pia huu ni wakati mwingine kwa mawakala wanaume kuhakikisha mnavivuka viunzi kwa wasichana wanaojiandaa kuwaweka mtegoni,” alisema Lundenga. 

Aliwataka mawakala hao pia kuhakikisha wanafanya mazungumzo na makampuni na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kusaka udhamini wa kufanikisha mashindano yao ambayo yanaania ngazi ya vitongoji, wilaya, mikoa na kanda. 

“Kuhusiana na zawadi pia mnatakiwa kuwa na makubaliano na washiriki kulingana na uwezo wako wakala…hata kama uko tayari kutoa jiko waeleze hivyo,” Lundenga aliongeza. 

Aliwaeleza pia mawakala hao kwamba mdhamini mkuu wa mashindano hayo ni
Redd’s Original ambayo imeahidi kutumia zaidi ya Sh. Milioni 500. Happiness Watimanywa ndiye mrembo anayetetea taji la taifa na mshindi wa pili, Latifa Mohammed pia walikuwepo jana katika semina hiyo inayotarajiwa kumalizika

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top