
Watanzania tunastahili kujikweza na kujipongeza kwa nafasi ambayo hivi sasa kwa upande wa burudani tunawika kona nyingi za dunia. Kwa kawaida tulizoea kushuhudia na kupigia kura wasanii tu lakini sasa PRODUCERS wanang'ara kwenye tuzo kubwa sasa.
Mfano mzuri kauonesha kijana mdogo huyu wa Kitanzania anayepeperusha bendera ya Tanzania kwa kupika kazi nzuri ya Diamond Platinum ya "My Number One". Hiki ni kibao ambacho naamini kabisa kinaitoa Tanzania kwenye sura tofati sana katika tasnia ya burudani, hakika tunastahiri kujipongeza kwa dhati Watanzania wote.
Kijana huyu, Sheddy ni moja ya watayarishaji wa muziki wanaowania tuzo za AFRIMMA huku ikiaminika kama kawa katika kundi gumu sana kwani anashindanishwa na tunaoamini ni wakongwe katika kazi hizo na wanamajina makubwa, ila si hoja kwetu katika kuhakikisha tunamrusha kidedea Mtanzania mwenzetu.
MASWALI YA KUJIULIZA YA MSINGI:
- Je, kwanini Sheddy kaingia kwenye tuzo?
- Je, anastahili?
- Je, tunapenda kushangilia ushindi huo?
- Je, tunapenda kuonesha uzalendo wa kweli?
- Ingia katika anuani ya afrimma.com
- Chagua NOMINEES
- Chagua Category unayotaka kuipigia kura
- Bofya jina unalotaka kulipigia kura
- Kisha bofya VOTE
ANGALIA MIFANO HAPA CHINI

(Huu ni mfano tu).
KUSHINDA AU KUTOKUSHINDA KWA SHEDDY:
Hakuna kikwazo au tatizo litakalotufanya sie ushindwe kumuinua kidedea kama tunajali hasa kazi zetu na mafanikio ya wazawa wetu. Si Sheddy tu bali Lady J dee, Mrisho Mpoto, Ben Paul na Diamond Platinum
KUMBUKA: Tusiishie tu kupiga kura, tujitahidi kutoa maoni pia (Comments) itasaidia sana.
KUPIGA KURA SASA BOFYA HAPA
"TANZANIA ITS OUR TIME"
