Featured
Loading...

Pesa iliyotumika kwenye video mpya ya Diamond na Iyanya London, kolabo na Davido tena?

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE


 

Wiki iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya kufanya show lakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofanya na msanii Iyanya wa Nigeria.

Alifunguka meneja Babtale ambae anasimamia kazi za Diamond sasa hivi ambapo amesema kutokana na kupiga hatua kwa Diamond na kuingia kwenye levo za kimataifa, imebidi waanze kufanya video za kiwango hicho cha kimataifa lakini haimaanishi kwamba ndio Platnumz hatofanya tena video Tanzania’
Video tuliyofanya na Iyanya Uingereza ni kwa sababu tulikua tunamuhitaji Director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake Uingereza ndio maana tukasafiri mpaka huko, kuna video ambayo tutafanya Nigeria tukishatoka Ghana na pia ikitokea kwamba tunatakiwa kufanya video Tanzania tutafanya hivyo. Alisema Babutale



Kuhusu gharama iliyotumika kufanya hii video Uingereza;
Bab Tale: kiukweli tunaumia, tunaumia kwa sababu kumlipa Moe Musa na kupata kila kitu kama kwenye hii video ya juzi tumemlipa Moe peke yake dola elfu 25 ambazo zinagonga mpaka milioni 40 za Kitanzania, bado usisahau tumewatoa kina Iyanya Nigeria kwa hela yetu kuwaleta London, kuwalipia nauli ya business class kwenye ndege na hoteli hawawezi kulala hoteli mbaya kama sisi watoto wa Manzese

Kwenye sentensi nyingine, Babtale ameithibitishia millardayo.com na AyoTV kwamba Diamond atasikika tena kwenye kolabo nyingine na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na Mafikizolo wa South Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV Afrika.

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top