Featured
Loading...

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYA YA KALIUA, AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE



 Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Wilaya ya Kaliua,katika ukumbi wa Millenium mkoani Tabora mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali za maendeleo ya miradi na hali ya kisiasa wilayani Kaliua. Kinana yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Usindi wakishuhudia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Zahanati ambayo tayari imwekwishakamilika,isipokuwa inasubiri kibali na kukamilika nyumba ya mganga.Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya

Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata taarifa fupi juu ya mradi wa ujenzi wa jengo la nyumba ya Mganga wilayani Kaliua katika kijiji cha Usindi,Kata ya Ushokora,Katika ziara hiyo ya siku 11,Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye,ambapo walipokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya .

 Katibu Mkuu wa CCM,dugu Kinana akilakiwa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya,mara baada ya kuwasili wilayani Kaliua,katika kijiji cha Usindi kata ya Ushokora akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye (hayupo pichani). mkoani Tabora.

Mbunge jimbo la Urambo Mashariki,Mh.Samwel Sitta akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi Prof.Juma Kapuya mapema leo kwenye wilaya ya Kaliua,mara baada uusindikiza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana aliyekuwa Wilayani Urambo Mashariki kwa ziara ya siku 11 ndani ya mkoa wa Tabora.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa katika kijiji cha Usindi,Kata ya Ushokora wilayani Kaliua mkoani Tabora mapema leo asubuhi,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye na kupokelewa na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya

 Ndugu Kinana pichani na viongozi wengine wa CCM,wakienda kukagua Mradi wa ujenzi wa Zahanati na nyumba ya Mganga,katika kijiji cha Usindi kata ya Ushokora wilayani Kaliua mkoani Tabora.

 Ndugu Kinana wat tatu kulia akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Urambo Magharibi,Mh.Prof Juma Kapuya,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenenezi Nape Nnauye na viongozi wengine wa CCM,wakitoka kukagua Mradi wa ujenzi wa Zahanati na nyumba ya Mganga,katika kijiji cha Usindi kata ya Usindi wilayani Kaliua mkoani Tabora. Picha na Jiachie Blog

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top