Dunia imeadhimisha siku ya kimataifa ya Nelson Mandela. Kumekuwa na shughuli mbalimbali za kijamii kumkumbuka rais huyo wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, aliyefariki dunia mwaka jana. Watu wametumia muda wa dakika 67 kufanya shughuli za kumkumbuka, ikiwa ni kukumbuka miaka 67 ya harakati zake za ukombozi. Salim Kikeke amekutana na wasanii kutoka Soweto waliokuwa wakifanya maonesho yao hapo London.
