
Tafuta Herufi ya Mwanzo ya jina lako na ushuhudie uhalisia wako, kama kweli tupe ushuhuda katika maoni hapo chini
(Nimeikuta sehemu katika mitandao ya kijamii)
HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa
mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu
mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda
Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu,
muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale
anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika
badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa
wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa
usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri
na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri
,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu.
Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye
mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu
na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G
mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye
imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua
matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali
ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na
nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake.
ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda
sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za
haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye
matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio
makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri.
mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia
za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na
hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo,
mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa
mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini
sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi
kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu,
hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra,
mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na
mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa
kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana
kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda
mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu
visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu,
wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto
mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi
makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda
ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio
baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati
kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye
tamaa na aliyekosa maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye
bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi,
wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni
watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa
kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na
kujitoa uaminifu.
HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda
Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na
husababishia kupoteza bahati katika maisha.
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda
matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya
kuamua jambo,
je na jina lako lina maana gani? Jibu usione aibu!






