
MAREHEM DEREVA WA SABENA...
Dereva alie kuwa anaendesha bus hilo wakati ajali inatokea hakuwa dereva alie toka na bus hilo mbeya. .. huyu ni fundi wa mabasi hayo ambae pia anagereji yake hapo mjini sikonge.. inasemekana basi la SASEBOSA limekuwa likiwasumbua sana SABENA hivyo fundi huyo ambae Zamani alikuwa akiendesha mabasi aliamua ashike stelingi kuwapa adabu SASEBOSA, inasemekana wakati akilipita basi la SASEBOSA wakiwa ubavu kwa ubavu makondakta, tani boi na tajiri aliekuwemo walikuwa wanashangilia ... maskini hakuona hata taa iliyowashwa na dereva wa SASEBOSA ikiashiria mbele kuna gari linakuja sekunde kadhaa baadae ikatokea ajali. .. Dereva halisi alikuwa siti ya nyuma kabisa kapumzika, katoka mzima R.I.P James Komba.
MAREHEM DEREVA WA AM..
Huyu amekufa kifo chakuumiza sana. .. Baada ya ajali alikuwa mzima kabisa ila alikuwa amebanwa sana kuanzia usawa wa kiuno ... miguu ikiwa nyang'a nyang'a... alikuwa akipiga kelele kuomba msaada lakini watu walishindwa kumsaidia hakukuwa na kifaa cha kukata vyuma ili wamtoe. .. maskini pengine maumivu makali Au. .akamua kuanza kubugia vipande vya vioo vilivyo tapaaka juu ya dashboard! alibugia kila mara mpaka uhai ulipo mtoka! mashine ya kukata vyuma ilifika saa 12 jioni toka ajali itokee sa6 na nusu. .. wakaambulia kutoa maiti yake tu. ..
LAWAMA KWA WATU WA SIKONGE...
Inasemekana hawa walipofika walikuwa wanajali abiria wa kwenye SABENA tu wale wa AM walisaidiwa walipofika watu wa TABORA MJINI...
CHANZO NI KUTOKA FACEBOOK KATIKA MOJA YA KUNDI KUBWA LA TABORA (TABORA NDIO KWETU)
<<>>
MIONGONI MWA VIFO HIVYO VILIHUSISHA WANACHUO CHA KILIMO TUMBI
<<>>






