Featured
Loading...

AJALI YA KUTISHA ILIYOTOKEA SABA SABA DARAJANI WILAYANI BUTIAMA- MARA

BOFYA VIDEO HAPO CHINI UONE MAMBO LIVE




eneo la tukio
Miili ya watu waliofariki katika jali ya mabasi ya Mwanza Coach na J4 Express eneo la sabasaba wilayani Butiama mkoani Mara,waliofariki ni zaidi ya 30,majeruhi zaidi ya 70

Mabasi yakiwa yamegongana

Wananchi wakiangalia bas la Mwanza Coach
Ndani ya moja ya mabasi hayo
***
MAELEZO: Malunde1 blog
Habari za hivi punde zilizokifikia chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba kuna ajali mbaya imetokea katika eneo la sabasaba Darajani wilayani Butiama mkoani Mara.

Inaelezwa kuwa ajali hiyo imehusisha magari matatu na kupoteza maisha ya watu zaidi ya 30 na kujeruhi watu zaidi ya 70 katika eneo la Sabasaba wilayani Butiama.

Ajali hii imetokea majira ya saa 5 na nusu ,Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara

Kufuatia ajali mbaya iliyohusisha magari matatu wilayani Butiama mkoani Mara

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Butiama Anjelina Mabula aliyezungumza na TBC muda mfupi uliopita amesema idadi ya watu waliopoteza maisha ni 38 hadi sasa huku majeruhi wakiwa ni 80.

Amesema ajali hiyo imehusisha basi la AM Coach lenye namba za usajili T736 AWJ likitoka Musoma kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi T677 CYC J4 Express likitoka Mwanza kwenda Tarime na gari jingine dogo aina ya Nissan Corola P332 KKT likitoka eneo la Sabasaba yote yalikutana kwenye mteremko yakitokea juu kwenda Darajani ,katika kupishana kutokana na spidi yao hawakuweza kupishana yakagongana na wakati huo gari hilo dogo lilipaki pembeni baada ya kuona hali tete nalo likagongwa kwa nyuma likasukumwa na kutumbukia mtoni.

Katika gari dogo kulikuwa na watu 8,wawili wamefariki dunia na majeruhi 36 kutoka kwenye mabasi hayo mawili nao wamefariki na majeruhi 80 wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Mara.

Madereva wote wamefariki dunia katika ajali hiyo mbaya

Ungana nami Sasa Upate Habari Moto Moto za Moja kwa moja Kwako
Bofya HAPA SASA U Like PAGE!

Share na Marafiki Post HiiPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Karibu tena
Get Free Email Updates to your Inbox!
© Copyright Mahaba Live
Back To Top