Ajali hiyo ilitokea tarehe 10 Oktoba, Ijumaa ya wiki iliyopita kwenye pori la kijiji cha Uluwila ambapo basi hilo lilikuwa linatokea Tabora kwenda Mpanda huku akiwemo msanii maarufu wa kundi la 2mbili wa Town BABA LEVO. Ajali hiyo ilihusisha basi la AM lililokuwa likitokea Tabora-Mpanda na inadaiwa kuwa dereva wa Coaster alikuwa akikwepa barabara mbovu na hivyo kuhamia upande ambao basi la AM lilikuwa likija na hivyo kugongana uso kwa uso.
Baba Levo amesema ameumia usoni na mwilini kwa kuchanwachanwa na vioo vya mbele vilivyopasuka kwenye basi.
“Baadhi ya abiria walifariki ambapo kati yao ni waliopasuka vichwa na shingo,”