Jengo la Machinga Complex likiwaka moto leo
Gari la zimamoto likizima moto huo
Moto ukiendelea kuwaka huku wananchi wa maeneo ya jirani wakiwa katika shughuli zao kama kawaida
Wananchi wakitazama madhara ya moto huo
Haya ndio maeneo yaliyokuwa yakichomelewa na mafundi hao
Tukio hilo limetokea mchana wa leo vizimba saba vya baadhi ya wafanya biashara vilivyopo ghorofa ya tatu.
Mpasha habari wetu kutoka jijini Dar es Salaam ameueleza mtandao huu wa matukiodaima kuwa chanzo ni cheche zilizotokana na kuchomelea moja ya kizimba kwa marekebisho yaliyokuwa yakifanywa na mafundi ambapo cheche hizo ziliangukia kwenye godoro lililokuwa kizimba cha pili na kusababisha moto ulioendelea hadi kizimba cha saba na kuteketeza mali mbalimbali zilizokuwemo.
Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwepo eneo hilo walifanya jitihada za kuuzima moto huo kwa kutumia vidhibiti moto ( fire extinguisher) na kutoa taarifa kwa zimamoto inayomilokiwa na kampuni ya Altimet walidai kuwa walifika kumalizia kuzima moto uliokuwa unaendelea kizimba cha saba,
Hata hivyo thamani ya mali zilizoteketea na moto huo bado kufahamika pia kutokana na tukio hilo wafanyabiashara wamepongeza jitihada za jeshi la zimamoto na uokoaji pamoja na ulinzi wa jeshi la polisi eneo hilo ..