Ni vifo tu Tanzania vinateketeza nguvu kazi za wajenga Taifa letu, kila kona matukio machafu ya kutisha, kusikitisha na kustaajabisha.

UPDATES
Basi la Sabena (T 110 ARV) lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza limegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline (T 803 ATN) lililokuwa likitokea Mwanza-Mpanda. Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka mjini wilaya ya Sikonge.
John Buswelu, kaimu mganga wa wilaya ya Sikonge akiongea kwa njia ya simu amesema amepokea maiti 17 na majeruhi 75. Vifo hivyo vinahusisha madereva wote. Hata hivyo shughuli ya kutafuta miili ilikuwa ikiendelea.
Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Komba aliyefariki papo hapo kiwiliwili tu ndio kilipatikana na juhudi za kutafuta kichwa ziliendelea na hali hiyo ilikuwa ngumu kutokana na kupondeka vibaya kwa gari la Sabena.
Baadhi ya wananchi wameongeza zaidi kuwa yawezekana hata madereva hao walikuwa ni Day-worker (Daiwaka) kama ilivyozoeleka.
Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mashuhuda wa ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria kati ya Sabena ya Mbeya-Mwanza na AM Dreamline ya Mwanza-Mpanda.




Baadhi ya miili ya marehemu.

PICHA NYINGINE
.jpg)
.jpg)
.jpg)