MAPENZI YA MZIWANDA NA SHILOLE
Shilole ambaye pia ni msanii maarufu nchini anayetikisa katika tasnia ya mziki wa hapa bongo amekuwa kwenye mahusiano matamu kati yake na Nuhu Mziwanda kwa kipindi kirefu huku yakiwa yanashamiri kila siku.
Katika hali ya usanii huu wa wapenzi hawa yawezekana sana kwa Mziwanda kuwa na star Shilole kungempa mashabiki wengi hasa katika mkoa wa Tabora ambako ndiko anakotokea mpenzi wake. Lakini hali ilikuwa ndivyo sivyo.
Shilole na mpenzi wake Nuhu Mziwanda |
Katika hali ya kufurahisha sana Shilole alitakiwa kumkaribisha kwa stage mpenzi wake na kumtambulisha kwa mashabiki wampokee kama shemeji yao. Basi bila mikwaruzo mpenzi wa Shish Baby alitumbuiza wimbo wake hadi mwisho.
"....wanangu eeeh mbona kama hamna mzuka niniii..., sikutarajia kama mngenifanyia hivyo shemeji yenu..... Sioni mizuka kabisaaaa....SHILOLE AINGILIA KATI
"....mnajua nini..! Nataka kumchukua dada yenu nimpeleke Iringa ama nini... eeeeh..! ....eeeh..!" Alisema Mziwanda. KELELE ZA MASHABIKI ZILIONESHA KUPINGA SUALA HILO
Baada ya kuonekana mume kama kapaniki akajitokeza Shilole na kusema na mshabiki moja kwa moja
"... sasa nyie mnamkataa shemeji yenu niliye mchagua mimi..? Basi nani ananifaa......." Alisema Shilole.
![]() |
DJ Zero wa Clouds |
Baada ya Shilole kuwauliza stajini mashabiki nani anamfaa kama wamemkataa shemeji aliyewatafutia mwenyewe, mashabiki walisikika wakitaja "...Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..! Zero..!". Ikawa sio ishu sana Shilole kawapa makavu live kuwa Nuhu ndiye mpenzi pekee ampendaye.
Ni baada ya kutia bonge la aibu kwa mashabiki akaamua tu kurahisisha mambo na kwakuwa pesa sabuni ya roho basi akamua kurusha pesa kwa mashabiki kitu kilichasababisha vurumai na kuleta zogo baina ya mashabiki wanaohangaikia kuokota pesa hadi kukata vizuizi hali ikaonekana si shwari, mamaaa Shilole akajitokeza kutetea hilo na kumtaka mmewe atulie na asipaniki aongee tu na mashabiki na kumsihi kuwa ni ndugu zake hao usirumbane nao.
Show ya Shilole ikaendelea.
ASHUKA JUKWAANI KWA HUZUNI
Mtandao huu ulimshuhudia Mziwanda akishuka bila mzuka hadi kukaa na kubaki akitafakari kama kuna kitu hajapendezwa nacho na mashabi wake.
ASHUKA JUKWAANI KWA HUZUNI
Mtandao huu ulimshuhudia Mziwanda akishuka bila mzuka hadi kukaa na kubaki akitafakari kama kuna kitu hajapendezwa nacho na mashabi wake.